Zaburi
117:1 Msifuni Bwana, enyi mataifa yote, Msifuni, enyi watu wote.
117:2 Kwa maana fadhili zake kwetu sisi ni kuu, Na kweli ya Bwana
hudumu milele. Msifuni BWANA.